Majaliwa alaani uovu unaofanywa kwa Wanahabari

LINDI: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amelaani vitendo viovu vinavyoendelea kuwakumba wanahabari ikiwemo vitisho, kutezwa nguvu na kufanyiwa vurugu katika kutekeleza shughuli zao za kila siku.
Katika kushughulikia hayo Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (HMTH), kushughulikia changamoto za wanahabari zikiwemo maboresho ya Sera ya Habari, kurefusha ukomo wa vitambulisho vya wanahabari (Press card), kuundwa kwa bodi ya ithibati, kuundwa kwa mfuko wa mafunzo kwa wanahabari na baraza huru la habari.
Akiwa mkoani Lindi katika Mkutano Mkuu wa Saba wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kiongozi huyo ameitaka wizara ya hmth kuunda kanuni katika maeneo yote yanayotakiwa kushughulikiwa pia iwahusishe wanahabari katika kutoa maoni ikiwemo Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF
“Kamilisheni mchakato wa kuunda bodi ile ya ithibati. Nataka bodi ipatikane mapema ili vyombo vingine kama baraza la wanahabari viweze kuanzishwa mapema iwezekanavyo,” ameagiza Waziri Mkuu.

3 comments

Comments are closed.