Majaliwa asifu upelekaji wa maji ngazi ya vitongoji

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameisifu Wizara ya Maji namna ilivyojipanga vizuri katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maji nchini kwa lengo la kufi kisha maji hadi kwenye vitongoji nchini.

Akifungua semina kwa wabunge kuhusu Sekta ya Maji, Dodoma jana alisema Wizara ya Maji kwa kujipanga huko moja kwa moja inatekeleza maagizo ya Ilani ya CCM pamoja na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyotoa wakati anafungua Bunge mwaka 2021.

Alisema Wizara kwa kuweka mpango kazi wake imeweza kutekeleza na kukamilisha miradi mipya na imekwamua miradi iliyokwama na kuhakikisha inafanya kazi na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

Kwa kutekeleza miradi hiyo, imesaidia binadamu na viumbe mbalimbali vinavyohitaji maji kupata huduma hiyo katika maeneo yao.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alisema wizara hiyo imejipanga vizuri kuondoa kadhia za maji nchini na imefanikiwa kutekeleza hilo kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha za kutosha katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maji nchini.

Aweso alisema wizara hiyo itahakikisha inatekeleza maagizo ya Ilani ya CCM ya kusambaza maji hadi ifikapo mwaka 2025 kwa asilimia 85 vijijini na mjini kufikia asilimia 95, akaahidi wizara hiyo kutokuwa kikwazo kufikia malengo hayo.

Habari Zifananazo

Back to top button