Majaliwa ataka ubia imara NHC, sekta binafsi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lichambue kwa umakini aina ya wawekezaji watakaoleta maombi ya ujenzi wa nyumba.

Aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizindua Sera ya Ubia ya NHC iliyofanyiwa marekebisho kwa lengo la kuweka uwazi na kuongeza tija katika miradi ya ujenzi wa nyumba baina ya shirika hilo na sekta binafsi.

“Serikali ingependa kuona wawekezaji na shirika mnajenga ubia imara utakaosaidia ukuaji wa sekta ya nyumba ambayo ni moja ya sekta muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi,” alisema Majaliwa.

Aidha, alilitaka shirika hilo kuhakikisha linasimamia ipasavyo miradi itakaloingia ubia na wawekezaji ili miradi itakayotekelezwa, itekelezwe kwa ufanisi na tija kwa taifa na mwekezaji husika.

“Serikali itakuwa karibu na tutakuwa na mkakati wenye tija wawekezaji wanaopata miradi ni wale wenye sifa na sio wale wawekezaji wababaishaji,” alieleza Majaliwa.

Pia, ameiagiza NHC kusimamia miradi iendane na thamani ya fedha iliyokusudiwa kuepuka majengo kujengwa kwa kiwango cha chini ikiwamo kuanguka na kuleta madhara kwa wananchi, lakini pia hasara kwa taifa.

Pamoja na hayo, alisema katika miji mingi ukiwamo Dar es Salaam, kwa sasa kuna majengo mengi na hakuna nafasi za kutosha za maegesho ya magari na kuagiza NHC katika miradi yake ya ubia na wawekezaji kujenga pia majengo ya maegesho ya magari.

Alieleza kuwa sera hiyo imefanyiwa maboresho makubwa ili kukidhi mahitaji na kuwa na tija kwa wawekezaji katika NHC jambo litakaloleta faida ikiwamo kuufanya ubia husika kuwa endelevu na wenye manufaa kwa umma.
“Kwa mfano, tangu kuanza kwa Sera ya Ubia miaka 2012 iliyopita, shirika limeingia mikataba 194 na sekta binafsi ambapo mikataba 73 ilifutwa kwa sababu ya ukiukwaji wa masharti, mikataba 111 yenye thamani ya shilingi bilioni 300, utekelezaji wake umefanyika ambapo mikataba 81 yenye thamani ya shilingi bilioni 240 utekelezaji wake umekamilika na mikataba 30 yenye thamani ya shilingi bilioni 60 utekelezaji unaendelea,” alieleza Waziri Mkuu.

Alisema serikali inatambua makazi ni jambo muhimu kwa maendeleo ya taifa, ndiyo maana imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ili kuwezesha sekta ya nyumba kuwa endelevu na yenye tija kwa wananchi na uchumi wa nchi.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa nchini kuna uhaba wa nyumba milioni tatu na mahitaji hayo yanaongezeka kwa wastani wa nyumba 200,000 kila mwaka.

Alibainisha kuwa upungufu huo unachangia wamiliki wa nyumba binafsi kutoza kodi kubwa na wakati mwingine kudai kodi ya mwaka mzima kwa mkupuo mmoja.

“Lengo la serikali ni kuwezesha wananchi wengi zaidi kumiliki nyumba zinazojengwa na shirika hili na waendelezaji wengine wa nyumba.

Kwa upande mwingine, Majaliwa alisema kumekuwepo na ongezeko kubwa la mikopo iliyotolewa ya uendelezaji miliki ikiwamo mikopo ya nyumba.

Alitoa mfano hadi kufikia Septemba, mwaka huu, NHC imewezesha benki na taasisi za fedha 33 kutoa mikopo ya nyumba ya Sh bilioni 147.7 kwa wananchi 6,177.

Alisema matokeo ya mafanikio hayo yamewezesha kuongezeka kwa mchango wa sekta ya miliki katika Pato la Taifa.

“Taarifa ya Hali ya Uchumi ya mwaka jana, inaonesha kuwa shughuli za kiuchumi za huduma za upangishaji

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x