Majaliwa atoa maagizo Mji wa Serikali

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza ifikapo Oktoba mwaka huu, majengo ya serikali yaliyopo Mtumba jijini Dodoma yawe yamekamilika ili azma ya serikali ya kuhamia kwenye majengo hayo ifikapo Januari Mosi, 2024 iwe itimie.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Julai 03, 2023 alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa serikali Mtumba.

“Tafuteni mbinu za kiufundi za kukamilisha majengo haya kwa wakati bila kuathiri viwango”moja ya mbinu ni kusimamia ujenzi huu usiku na mchana, tunataka tumalize majengo haya, Watanzania wanataka kuona majengo yanakamilika na kutumika.” Amesema Majaliwa.

Waziri Majaliwa amewataka wasimamizi wa ujenzi wa majengo hayo watumie bidhaa zinazozalishwa na viwanda vilivyopo nchini.

“Rais Dk Samia amesisitiza kuhusu uwekezaji na amekuwa akialika wawekezaji wa nje na wa ndani kujenga viwanda vya bidhaa mbalimbali hapa nchini ikiwemo marumaru (tiles). Tutumie bidhaa zao badala ya kuagiza bidhaa hizo kutoka nje.” Ameongeza Majaliwa.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button