Majaliwa atoa maelekezo kukabiliana na El-Nino

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kuchukua hatua stahiki kukabiliana na mvua za El-Nino sambamba na kujiandaa kukabiliana changamoto hiyo.

Akizungumza leo Novembea 10, 2023 katika hotuba ya kuahirisha shughuli za bunge Mkutano wa 13, Kikao cha 10 cha Bunge, Majaliwa ameziagiza wizara, mikoa na taasisi za serikali kuainisha na kuandaa rasilimali za kujiandaa, kuzuia na kukabiliana na maafa.

Majaliwa ameitaka wizara, mikoa na taasisi za serikali kuelimishaji namna ya kuwahamisha wananchi kwenye maeneo hatarishi na kuchukua tahadhari ili kuokoa maisha na mali.

Kiongozi huyo amezitaka idara na taasisi zinazohusika na mazingira na miundombinu kuhakikisha barabara zinapitika wakati wote, mitaro na makalavati yanazibuliwa, kuimarishwa na kusafishwa ili kuruhusu maji kupitika kwa urahisi.

Amezitaka sekta za maji, umeme na mawasiliano kuweka mipango ya kuzuia madhara, lakini pia kushirikisha wadau wa maafa wakiwemo wananchi , taasisi za umma na sekta binafsi katika mipango ya usimamizi wa maafa.

“Kamati zote za maafa katika ngazi za kijiji, wilaya, mkoa na taifa, zianze kujipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto za El-Nino endapo zitajitokeza kwenye maeneo yetu.” Amesema Majaliwa.

Sambamba na hilo amezitaka wizara, idara na taasisi, mikoa na halmashauri kuandaa mipango ya utekelezaji katika maeneo yao kwa kuzingatia mpango wa taifa wa dharura kukabiliana na El-Nino.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button