Majaliwa aungana na Rais Samia maombolezo kifo cha Lowassa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameungana na Rais Samia kuomboleza kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

Katika ujumbe wake aliochapisha kwenye mitandao ya kijamii leo Februari 10,2024, Majaliwa amesema taifa limepata pigo kubwa kwa kumpoteza kiongozi huyo.

“Kwa hakika nchi yetu imepata pigo kubwa kutokana na msiba huu mzito, kwakuwa Mhe. Edward Lowassa alikuwa Kiongozi aliyehudumu kwa juhudi na maarifa makubwa katika nafasi zote alizowahi kuzishika ikiwemo ya Uwaziri Mkuu.” Ameandika Majaliwa.

Advertisement

Aidha ametoa pole kwa familia, Wanamonduli na Watanzania wote kwa msiba huo.