WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amefika soko la Kariakoo na kuwasihi wafanyabiashara wasitishe mgomo wao na wafungue maduka, ombi ambalo limekubaliwa na wafanyabiashara hao
Majaliwa amefika Kariakoo mchana huu Mei 15,2023 baada ya wafanyabiashara hao kuweka mgomo na kutofungua maduka yao wakilalamikia utitiri wa Kodi.
Akizungumza Majaliwa amesema “Soko la Kimataifa tunalitegemea kuingiza mapato makubwa serikali kupitia tra lazima tulitunze, Msumbiji, Malawi, Congo, Uganda, Kenya leo kulifunga sio sawa.
“Nimeona ujumbe wenu kupitia mabango nimesoma moja baada ya moja, kuna moja linasema TRA imefukuza wageni wetu, hili jambo ni serious, jukumu la serikali ni kuhakikisha inasimamia vizuri wafanyabiashara wafanye biashara zao vizuri. Tunatambua mchango wenu kwenye nchi hii. “Amesema
Amesema ataita wafanyabiashara wa Mikoa ya Mbeya, Arusha, Mwanza, na Dodoma na Dar es Salaam kesho kutwa Jumatano ili kusikiliza kero zao.
“Wakati changamoto zenu zinashughulikiwa fungueni maduka muendelee na biashara, ili msiuwe soko letu, maana wafanyabiashara wa nje wanakuja kununua mizigo wakisikia mmegoma w wanahairisha tiketi zao.
Nae Martin Mbwana Mwenyekiti wa Wafanyabiashara akizungumza kero kubwa inayowasumbua ni ushuru wa forodha, na kuitaka TRA ufanye makadirio ya usahihi na weledi
“Tunawaomba TRA wafanye makadirio kwa usahihi na weledi, wanavyotufanyia inachangia kutotoa risiti ya EFD.” Amesema na kuongeza
“TRA imegeuza Kariakoo shamba la bibi kila siku wanakuja na tozo mpya mara ya stoo, mara sijui ya nini, kuna vitengo sita Kariakoo.
“TRA inadharau wanasiasa, Mkuu wa Mkoa akiagiza wanapuuza wanasema lete barua ukipeleka barua wanakwambia uyo mwanasiasa…hawatekelezi.
“Mama Samia (Rais) alizungumza Kaitaba June mwaka jana alisema Kodi za miaka mitano zifute tukashangilia na kupiga makofi lakini TRA wanasema hajazungumza, ni kauli za kisiasa tulete barua, TRA wamegeuza shamba darasa.” Alisema Mbwana kauli ambayo ilimchefua Waziri Mkuu Majaliwa ambae alifoka na kusema kila lililotamkwa na Rais, Makamu wa Rais, ni agizo.
“TRA Rais kasema kodi za miaka mitano zifutwe nyie mnasema leta barua, mfanyabiashara wa Kariakoo anapata wapi barua ya Rais? ” amehoji .
“Ningemjua uyo aliyesema anataka barua ya Rais ningemshughulikia mara moja. Agizo la Rais Makamu wa Rais, Waziri Mkuu ni maagizo yakitolewa wachini ni kutekeleza
Aidha, Waziri Mkuu ameagiza mikosi kazi kinachokusanya mapato kisitishe mara moja.
“Kikosi kazi kilichoundwa cha tra, pamoja na kazi nzuri ya kukusanya mapato, Rais alikataza vikosi kazi kwa sababu vinasumbua wafanyabiashara na wakati mwingine vinatumika kuchukua rushwa.
“Kamishna wa TRA, Kamishna mambo ya ndani hivyo vikosi kazi visitishwe mara moja, na kama kuna ulazima Waziri wenu wa fedha hajue.
“Tarehe 17, nitakutana nanyi Anatoglo tutaiangalia hiyo task force hii inayoendesha kamatakamata kila siku.
“Kamishna wa mapato ya ndani, kanuni zipo, Rais alishasema Kodi zitafutwe kistarabu, wapeni elimu, kamatakamata mtaua biashara, imarisha kitengo chako cha elimu.
Kuhusu tozo ya stoo, Majaliwa anemuagiza Kamishna wa TRA kuumiza kichwa na kutoa Suluhu mbadala.
” Usajili wa stoo za mizigo, bandarini waleta mizigo wana utaratibu wao, mizigo midogo inawekwa kwenye kontena la mtu mmoja risiti mnatoa ya mtu mmoja, hao wadogo hamuwapi, nenda kaumize kichwa uje na utaratibu mzuri, ili mdogo nae kodi yake ionekane asisumbuliwe na wewe….; “Mbaya sana kwa taasisi ya serikali kupigiwa kelele suala la rushwa.
Majaliwa: Unapoombwa rushwa toeni taarifa Polisi
Wafanyabiashara: Hatutakii…. hapanaaa
Majaliwa: RPC .. umeona hiii?
“Hii maana yake nini watanzania hawana imani na mifumo yenu. Jeshi la Polisi msaidie sana hawa wafanyabiashara ikiwezekana muwakamate waomba rushwa.
Sheria mpya Stock (Uhifadhi)
Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza sheria hiyo isitishwe mara moja.
“ilikua na nia nzuri kujua biashara gani imeingia nchini, ila hii pia isimamishe kwanza, tutoe elimu. Sitisha tujipange ili tujue malengo kwa kipindi kifupi tuliyoitumia yamefikiwa?.
“Tabia ya kuonea wafanyabiashara mkome mara moja. Mambo mengine yanapelekea kujenga mambo mabaya kati ya mlipa Kodi na mtoza Kodi.
“Wamesema mengi wengine mtaji umekufa, wengine wanaenda m?kufanyabiashara nje, wanandikisha kontena la vitenge linaenda Zambia alafu linarudi nyuma nyuma, tra wasaidieni wafanyabiashara wafanye biashara kwa uhuru.
” ‘Zungu’ kwa kuwa ni Naibu Spika uwezi kusema ila umewatuma waseme ujumbe wako tumeupata.
“Tulishaagiza Kariakoo biashara zifanyike mpaka usiku saa 24 lakini mpaka sasa halijatekelezwa, hili nalo nitakuchukulia hatua.
“Nawasihi mkubali kufungua biashara nitakutana nanyi Jumatano, kesho naenda kumuwakilisha Rais kumzika Membe haitakua busara serikali isipokuwepo wakati alikua Waziri kwa miaka mingi
“Nawasihi sana fungueni biashara sasa hivi hata mpaka asubuhi,”
“Tutaiangalia alitamka mwaka gani turarudi nyuma utekekezaji uanze, tra, RAIS uwa andiki barua atandika barua ngapi? kila agizo ni kutekeleza.
Nae, Mbunge wa Ilala Musa Hassan ‘Zungu’ amesema wale wote waliokejeli kauli ya Rais kuwa ni siasa watawaita Dodoma Kujieleza