Majaliwa azindua benki ya TADB Kanda ya Kusini

Atoa maagizo tisa

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Kanda ya Kusini huku akitoa maelekezo tisa kwa wakulima na uongozi wa TADB

Akizungumza katika uzinduzi huo Majaliwa amesema  Benki hiyo  inalenga kusimamia mapinduzi katika sekta ya kilimo.
Amesema, kwa takwimu zilizopo serikalini,  sekta ya kilimo inatoa ajira ya wastani wa asilimia 75 ya watanzania wote kuchangia kwa   asilimia 100 ya chakula kinachozalishwa nchini na zaidi ya asilimia asilimia 65 ya malighafi inayopelekwa viwandani.
Kufuatia hali hiyo, Majaliwa ametoa maagizo tisa kwa uongozi wa Benki ya TADB pamoja na wakulima, wavuvi na wafugaji.
Kwanza amesema, benki hiyo imeanzishwa ili kutoa unafuu kwa wakulima, wafugaji na wavuvi kunufaika na mikopo ya muda mrefu, mfupi na wa kati.
“Naiagiza Management ya TADB kusimamia kwa weledi malengo ya kuanzishwa kwa benki hii Tanzania….; Tangu kuanzishwa  benki hii imekua na manufaa kwa mtu mmoja mmoja na vikundi.
“Tayari watu 1, 657,494, 000 wameshapata mikopo TADB sambamba na vikundi 207.
“Haya nayoyasema yanaweza yakawa hayajawagusa wana Mtwara, Lindi na Ruvuma, kwa sababu benki hii huduma zake zilikuwa mbali, natumaini kuanzishwa Kanda hii ya Kusini huduma zitaongezeka mara dufu.”Amesema.
Pili amewataka wana Kanda ya Kusini kutoka kwenye Kilimo cha kujikimu na kwenda kwenye Kilimo cha biashara ili kuongeza mnyororo wa thamani.
“Benki ya TADB imetenga sh bilioni 35 kwa ajili ya kuwakopesha wakulima wa korosho ili kuendeleza zao hili. Ni matumaini yangu fedha hizi na nyingine ambazo zitawekwa zitachangiza maendeleo ya serikali.
“Changamkieni fursa kupata uwelewa zaidi, mkapate elimu ya kilimo cha kisasa,elimu ya mikopo, mtakapokopa mlipe ili wengine nao wakope.
Pia,  manejimenti ya Benki wametakiwa kuweka masharti nafuu katika kutoa mikopo kwa wakulima, wavuvi na wafugaji ili kila mmoja aweze kupata huduma.
“Angalieni riba mnayotoza iwe ndogo ili wakulima, wafugaji na wavuvi wamudu kufanya biashara na kuweza kurejesha mkopo
Pia, nawaagiza maafisa biashara wa Benki wekeni utaratibu wa kuwatembelea wakulima, kuona miradi yao na kusimamia vizuri fedha zilizowekwa.
“Nunueni gari la sinema watu watavutiwa kulisogelea, mtoe elimu.
“Wakulima, wafugaji na wavuvi fanyeni matumizi sahihi ya fedha kwa miradi iliyokusudiwa na yenye  tija,  mkitumia vinginevyo hutozalisha na hutopata faida na kurejesha mkopo.”Amesema
Amewataka , uongozi wa TADB kuweka utaratibu wa kujitangaza na kutoa  na elimu ya mikopo
Majaliwa ameitaka Wizara ya Kilimo,  na uvuvi kuweka utaratibu mahususi kwa vijana kujiandikisha kwenye programu mbali mbali ili waweze kupata mafunzo ya ufugaji na uvuvi wa kisasa, wanufaike na mikopo na waweze kujiajiri.
“Watafutieni  fursa za masoko,  shirikianeni na mabalozi ili wakulima, wafugaji na wavuvi waweze kupata masoko ya nje, kwa kufanya hivyo mtainua uchumi wa mmoja mmoja na wa taifa. ” Amesema Majaliwa na kuongeza
” Vile vile  ili kuongeza ajira pamoja na kuchukua hatua kuhakikisha pembejeo za Kilimo zinapatikana kwa wakati na kwa gharama nafuu. “Amesema
Amesema, pia kubainisha fursa za masoko zilizopo ndani na nje ya nchi.
“Benki yetu hii, inahudumia pia sekta ya uvuvi na ufugaji. Kwa kuwa suala la usafiri na usafirishaji ni muhimu kwa mazao, serikali inaimarisha miundombinu ya usafirishaji ikiwemo barabara, ujenzi wa reli wa kisasa, reli ya kati, na mpango wa serikali ni kujenga reli ukanda wa Kusini Mtwara Corridor.
“Itumieni vizuri fursa zinazotolewa na benki hii, serikali imeweka mkakati wa kuwawezesha vijana kulima kupitia program ya kesho iliyo bora, kwa kuanzia tumechukua vijana 812 na kuwaingiza kwenye Kilimo na kuwafundisha mbinu nzuri za Kilimo bora kulingana na aina ya udogo alionao.

Habari Zifananazo

Back to top button