Majaliwa: Daraja la JPM litakamilika kwa wakati

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema miradi yote ya kimkakati itakamilika kwa wakati na hakuna mradi utakaokwama.

Amesema kauli hiyo leo, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa  Daraja la JPM lenye urefu wa Kilomita 3.2  na barabara unganishi yenye urefu wa Kilomita 1.66. Daraja lipo wilayani Misungwi (Kigongo) na Busisi ipo wilayani (Sengerema) mkoani Mwanza.

“Hakuna mradi wa kimkakati utaokaokwama, nawaondoa shaka. Tuliahidi na tunatekeleza na Rais Samia anaendeleza miradi yote.Daraja hili litakamilika kwa muda uliopangwa nawaahidi,” alisema Majaliwa na kuwataka Wakala wa Barabara (Tanroads) kuhakikisha daraja hilo linakamilika kwa wakati.

Amesema jukumu la serikali ni kuwafikia wananchi, huku akipongeza asilimia kubwa ya wakandarasi waliopo katika mradi wa daraja la JPM ni Watanzania.

“Sasa Watanzania tunapata taluuma ya ujenzi wa daraja. Nchi yetu ina uwezo wa kujenga daraja kama hili sehemu yoyote,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Habari Zifananazo

Back to top button