WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameipongeza klabu ya Yanga kufuatia ushindi wa mabao 5-1dhidi ya Simba SC, mchezo uliopigwa Novemba 5, 2023 uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Majaliwa ametoa pongezi hizo leo Novemba 10, 2023 bungeni jijini Dodoma alipolihutubia Bunge wakati akiahirisha mkutano wa 13, kikao cha 10 cha Bunge la Tanzania.
“Niipongeze timu ya Yanga kwa kushinda mchezo wa juzi.”
Waziri Mkuu pia ameipa pole Simba SC kwa kufungwa magoili matano na watani zao Yanga.