Majaliwa kuongoza marathon kuchangia Watoto njiti
WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za hisani zilizoandaliwa na Benki ya Maendeleo Benki zenye lengo la kusaidia hospitali ya KCMC kwa watoto Njiti na kituo cha watoto wenye usonji Mtoni Mtongani
Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Septemba 2,2023 katika uwanja wa Farasi jijini Dar es Salaam
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya usimamizi wa hatari na taratibu, Peter Tarimo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 9,2023 Dar es Salaam
“Benki inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake katika kusherehekea imeaandaa mbio za hisani ( Maendeleo Bank Marathon) mgeni rasm akiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.”Amesema Tarimo na kuongeza
” Mbio hizi zina kauli mbiu “Hatua ya Faraja” fedha zitakazopatikana zitaelekezwa hospitali ya KCMC kwa watoto Njiti na kituo cha watoto wenye Usonji kilichopo Mtongani.”Amesisitiza