Majaliwa: Madiwani Ileje acheni malumbano

SONGWE: WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje waache malumbano na badala yake wafanye kazi kwa pamoja.

“Tumeleta fedha Sh. bilioni 2 za ujenzi wa jengo la halmashauri tangu mwaka jana lakini ninyi bado mnabishana mjenge wapi jengo hilo. Au mnataka nizirudishe hizo fedha?” alihoji na kujibiwa hapana.

“Tumeleta fedha mjenge jengo jipya lakini ninyi mnataka mbomoe lililopo ili mjenge jingine wakati hapo hakuna eneo la kutosha kupanua mji wenu. Serikali imegoma msibomoe hayo majengo, na badala yake mnatakiwa mwende kujenga eneo la nyumba 10,” alisema.

Advertisement

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo Novemba 23, 2023 wakati akizungumza na watumishi, wakuu wa idara, viongozi na wakuu wa taasisi walioko wilayani Ileje kwenye kikao cha watumishi kilichofanyika katika ukumbi wa RM, Ileje, mkoani Songwe.

Alisema madiwani wana nguvu zote kwenye halmashauri lakini ni lazima pia wasikilize ushauri unaotolewa na watalamu.

 

3 comments

Comments are closed.