Majaliwa: Mapato robo ya kwanza Sh tri.9.6

KATIKA kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2023/2024, mapato kutoka vyanzo vyote vya ndani na nje yalifikia Sh trilioni 9.06, sawa na asilimia 89.6 ya lengo la kipindi hicho, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema.

Akizungumza leo Novembea 10, 2023 katika hotuba ya kuahirisha shughuli za bunge Mkutano wa 13, Kikao cha 10 cha Bunge, Majaliwa amezielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato na kuimarisha mifumo ya udhibiti wa ndani ili kuondoa mianya ya uvujaji wa mapato.

“Aidha, niwasihi watumishi wote waliopewa dhamana hiyo kutekeleza jukumu hilo kwa uadilifu na kuendelea kutoa elimu ya mlipakodi ili kufanikisha ulipaji wa kodi kwa hiyari.” Amesema Majaliwa.

Advertisement

Majaliwa amewapongeza watumishi wa taasisi zenye dhamana na ukusanyaji wa mapato zikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kufanikisha ukusanyaji huo.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *