Majaliwa: Mvua zitaendelea hadi Mei

DODOMA: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kulingana na utabiri wa hali ya hewa unaonesha kuwa mvua za masika zitaendelea kunyesha hadi Mei, 2024.

Majaliwa ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo Aprili 25, 2024, wakati akitoa Tamko la Serikali kuhusu matukio ya hali ya hewa nchini, ambapo amesema ongezeko la joto duniani limesababisha uwepo wa El-Nino ambayo imeambatana na mvua kubwa zilizosababisha mafuriko.

 

Advertisement

Amesema mwezi Oktoba hadi Desemba 2023 kulikuwa na ongezeko kubwa la mvua, ambapo jumla ya milimita 534.5 zilipimwa ikilinganishwa na milimita 227.2 kwa mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 135.

Pia amesema ongezeko hilo la mvua kubwa limeshuhudiwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Aprili 2024.