Majaliwa: Sensa imefanikiwa asilimia 99.9
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema zoezi la Sensa ya Watu na Makazi limefanikiwa kwa asilimia 99.9.
Akizungumza katika katika hafla ya matokeo ya awali ya Sensa leo Oktoba 31,2022 mjini Dodoma, Majaliwa amesema zoezi hilo limekua na ufanisi mkubwa kuliko sensa zote zilizowahi kufanyika nchini.
Kufanya Sensa ni kazi kubwa na ghali sana, hata hivyo, nchi zote duniani hufanya sensa kutokana na umuhimu wake.” Amesema Majaliwa
Amesema kupitia Sensa hupatikana taarifa muhimu za kutumiwa na serikali kupanga mipango ya maendeleo ndani ya nchi kwa lengo la kuwahudumia wananchi.
Nae, Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara, Anna Makinda amesema matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi yaliyozinduliwa leo ni matokeo ya mwanzo yanayotokana na uchambuzi wa maswali machache kati ya 100 yaliyokuwepo katika dodoso.
Amesema kadri uchambuzi utakavyokuwa unakamilika ndivyo matokeo yatakavyoendelea kutolewa kwa mujibu wa kalenda ya kuchapisha matokeo ya Sensa.