Majaliwa: Serikali itaendelea kutekeleza miradi yote

SERIKALI imeeleza kuwa itaendelea kuwajibika katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na maeneo yaliayoainishwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuimarisha huduma kwa wananchi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo leo katika Mkutano wa 10 wa chama hicho, unaoendelea jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya Serikali ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika miradi ya maendeleo.

Majaliwa amesema Serikali itaendelea kushughulikia changamoto na kwamba Serikali itaendelea kupokea maelekezo ili kuimarisha utendaji kazi ndani ya serikali, utendaji wenye uadilifu na uaminifu.

Waziri Mkuu amemhakikisha Rais Samia kuwa wao kama watendaji wa Serikali wataendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na kupokea maelezo, uadilifu na uaminifu wa hali ya juu.

“Mh Mwenyekiti Tumeona kazi zako na tunaaendela kuamini kazi hizi zitaboreshwa uendelee kufanya kazi kwa amani na utulivu, wasaidizi wako tupo,” amesema Waziri Majaliwa.

Habari Zifananazo

Back to top button