#BREAKING: Mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Jesus atakosa mechi zote za Kombe la Dunia, baada ya kupata jeraha la goti katika mchezo wa jana dhidi ya Cameroon.
Taarifa hiyo imetolewa na timu ya madaktari wa Brazil, ambapo Alex Telles naye atakosa michezo yote kutokana na majeraha.
Jesus atarejea Arsenal Januari, huku taarifa zikieleza kuwa huenda akakaa nje kwa mwezi mmoja, hali inayohofia pengine akakosa michezo ya Ligi Kuu ya England, itakayoendelea Disemba 26 mwaka huu.
Mchezo wa kwanza baada ya kumalizika kwa kombe la dunia, Arsenal itakutana na West Ham United.