Majeruhi ajali Arusha kutibiwa bure

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema majeruhi wa ajali iliyotokea jana eneo la Ngaramtoni mkoani Arusha watatibiwa bure.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel ametoa taarifa hiyo leo alipotembelea majeruhi hao katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mount Meru.

Dk Mollel amesema majeruhi wote wanaendelea vizuri ila mmoja kapewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC mkoani Moshi.

Advertisement

Pia ametoa wito kwa wananchi wa Arusha na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu wakati wakiendelea kuwatibia majeruhi na kwa wale waliopoteza ndugu zao utaratibu wakupatiwa miili unaandaliwa na wataalamu.