Majeruhi waliosalia maafa Hanang ni 14

MANYARA: Serikali imeeleza maendeleo ya hali baada ya maafa ya maporomoko ya tope, mawe, magogo na maji kutoka Mlima Hanang wilayani Hanang mkoani Manyara, yaliyotokea alfajiri ya Desemba 3, 2023.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 15, 2023 imeeleza kuwa Idadi ya majeruhi inaendeelea kupungua wilayani Hanang mkoani Manyara ambapo sasa wamebakia majeruhi 14 kutoka idadi ya jumla ya 139 waliofikishwa hospitalini baada ya maafa kutokea.

Akiwasilisha taarifa hiyo Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi ameeleza kuwa hadi sasa waathirika 36 ndio waliobakia kambini.

Advertisement

Matinyi ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuwaunganisha waathirika na ndugu zao na tayari waathirika 460 kutoka kaya 133 wameshaunganishwa na ndugu na jamaa zao hadi kufikia leo.

Ameongeza kuwa kila mtu au kaya inayoondoka kambini inapewa chakula na mahitaji muhimu ya walau siku 30 ili kuwasaidia waendelee na maisha.

Aidha ameeleza kuwa kiasi cha Sh 4,749,757,500/- zimeshakusanywa hadi kufikia sasa

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *