Maji hayajarudi Gaza
WIZARA ya mambo ya ndani ya Gaza imeeleza huduma za maji hazijarejeshwa katika eneo hilo.
“Wakazi wanakunywa maji yasiyo na afya, na kusababisha hali mbaya ya kiafya inatishia maisha ya raia,” msemaji wa wizara hiyo, Iyad al-Bozom alisema.
Katika taarifa iliyotolewa leo na mtandao wa Al-Jazeera imeeleza kuwa kwa siku 10 zilizopita, hakuna maji safi yaliyokuwa yametolewa na Israeli.