MOROGORO Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Maharage Chande amewaomba watanzania kuombea nchi ipate mvua za haraka ili kuvinusuru vituo vya umeme ambavyo mabwawa yake yameanza kupungukiwa na maji ya kuzalisha nishati hiyo kwa viwango vyake.
–
“Kuna changamoto ya kupungua kwa maji katika mabwawa ya Mtera, Kihansi na Kidatu. Kama mvua za vuli zitachelewa uzalishaji wa umeme utapungua katika mabwawa hayo,” amesema.
–
Akizungumza mbele ya kamati ya bunge ya Nishati na Madini baada ya kutembelea hali ya uzalishaji wa umeme katika bwawa la Kidatu, Chande amesema kukua kwa uwekezaji kumeongeza pia matumizi ya umeme.
–
“Vituo vyetu vya kuzalisha umeme vinafanya kazi vizuri, tuombe mvua zinyeshe mapema ili uzalishaji usiathirike, vinginevyo tutapata upungufu,” amesema.
–
Awali Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amemshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan akisema dhamira yake ya kufikisha umeme kwa watanzania wote inaendelea kudhihirika.
–
Amewatoa hofu watanzania na kuwataka kutunza na kulinda vyanzo vya maji amesema vyanzo vya umeme vinajitosheleza na vinafanya kazi kwa ufanisi.
–
Amesema Juni 2024 Tanzania itakuwa na umeme wa uhakika zaidi kwani bwawa la Mwalimu Nyerere linatarajiwa kuanza uzalishaji wake.
–
Comments are closed.