Makaburi ya kipunguni kuhamishwa

DAR ES SALAAM: HALMASHAURI ya jiji la Dar es Salaam (DCC) kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inatarajiwa kuhamisha makaburi ya Kipunguni na kuyapeleka katika eneo la Mwanagati Kata ya Mzinga.

Taarifa ya Mkurugenzi wa jiji (DCC), JOMAARY Satura imesema kuwa makaburi hayo yanahamishwa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege Mtaa wa Kipunguni kata ya Kipawa na zoezi hilo litasimamiwa na wataalamu kutoka halmashauri ya jiji la Dar es Salaam wakishirikiana na wataalamu kutoka TAA.



Amesema kuhamishwa kwa makaburi hayo ni kwa kuzingatia kanuni ya 46 (1) na 46 (2)(C) za kanuni za serikali za mitaa, mamlaka ya miji, udhibiti wa maendelezo za mwaka 2008.

“Hivyo wananchi wote wenye ndugu au jamaa waliozikwa eneo hilo wafike ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kipawa kujiandikisha wakiwa na barua ya utambulisho kutoka ofisi ya serikali ya mtaa anaoishi.”Amesema


Amesema, zoezi hilo la kujiandikisha litafanyika kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Septemba 20 hadi Desemba 20, 2023.

Habari Zifananazo

Back to top button