Makadirio bajeti Wizara ya Maji bilioni 627.77

DODOMA: Wizara ya Maji imeomba Bunge lipitishe  jumla ya Sh bilioni 627.77  makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa ajili ya matumizi  kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo leo, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema  Sh bilioni 69. 66 ni fedha za matumizi ya kawaida na Sh bilioni 558.11 ni fedha za maendeleo.

Amesema, kati ya fedha za matumizi ya kawaida, Sh bilioni 17.54 ni kwa ajili ya kugharamia matumizi mengineyo (OC) na Sh  bilioni 52. 12 ni kwa ajili ya kulipa mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara, RUWASA, Mfuko wa Taifa wa Maji na Chuo cha Maji.

Advertisement

Aidha, amesema kwa upande wa fedha za maendeleo, Sh  bilioni 340. 46 sawa na asilimia 61 ni fedha za ndani na Sh bilioni 217.65 sawa na asilimia 39 ni fedha za nje.