Makalla amrithi Makonda CCM

DAR ES SALAAM: KITENDAWILI cha mrithi wa Paul Makonda kimeteguliwa baada ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumteua, Amos Makalla kurithi viatu vya Makonda katika nafasi ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya chama hicho.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, iliyoketi saa 10:00 alasiri leo Aprili 3, 2024 pamoja na mambo mengine imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kuwachagua wajumbe ambapo mbali na Makalla pia imemteua, John Mongella kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichukua nafasi ya Anamringi Macha ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Pia, Ally Hapi, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania, akihukua nafasi ya Gilbert Kalima ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga wakati Jokate Mwegelo ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM akichukua nafasi ya Fakii Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Habari Zifananazo

Back to top button