Makalla: zaidi ya asilimia 94 ya wakazi DAR wamehesabiwa

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema Mkoa huo umefanya vizuri kwenye zoezi la Sensa ya watu na Makazi ambapo mpaka asubuhi ya leo Agosti 30 zaidi ya asilimia 94.3 ya Wananchi walikuwa wamehesabiwa kulingana na taarifa zilizotumwa na Makarani wa zoezi hilo.

Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya mwenendo wa zoezi hilo, RC Makalla amesema Makarani ambao bado hawajakamilisha kutuma taarifa wakituma taarifa zote ni dhahiri kuwa Mkoa utakuwa umefikia asilimia 100.

Aidha RC Makalla amesema Mkoa huo unafanya Zoezi hilo kwa umakini mkubwa ili kupata takwimu sahihi na za uhakika Kutokana na Mkoa huo kuchukuwa asilimia 10-13 ya Wananchi wote wa Tanzania.

Ili kuhakikisha kila mmoja anahesabiwa, RC Makalla amewataka Wananchi ambao bado hawajahesabiwa kufika Ofisi za Serikali ya mtaa na kuacha mawasiliano au kupiga simu kupitia namba maalumu zilizotangazwa kwa kila Wilaya ili aweze kuhesabiwa.

Pamoja na hayo RC Makalla amempongeza Kamisaa wa Sensa Anna Makinda kwa kuongeza siku ambapo pia amewapongeza Wakuu wa Wilaya kwa kusimamia vizuri zoezi hilo.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
gahsg
gahsg
1 year ago

Majina ya IDARA NANI KAKOSEKANA – Kazi ya matajiri!?
mavula
dines
mabuma
robert
aloys
godfrey
marry
maganya
robiey
sanga
tibi
fred
haule
cheche
Milka
Magret
mwakanema

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x