Makamishna wapya TFS watakiwa kuzingatia weledi

Makamishna wapya TFS watakiwa kuzingatia weledi

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Brigedia Jenerali, Mbaraka Mkeremy, amewataka makamishna wapya 47 wa uhifadhi kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi, ikiwemo kukabiliana na changamoto za uharibifu wa misitu.

Pia amesisitiza mafunzo ya uongozi waliyoyapata yaimarishe utendaji kazi wa kila siku, ili kudhibiti matukio mbalimbali ya uharibifu wa misitu.

Agizo hilo amelitoa leo, wakati wa kuhitimisha mafunzo ya uongozi wa maofisa wa TFS na kusititiza uzalendo kwa wakala hao, ili kutetea nchi na kulinda rasilimali zilizopo.

Advertisement

Amesema mafunzo hayo yalete mabadiliko ya utendaji kwa watumishi wenzao, ikiwemo kubainisha masuala muhimu ya kufanyia kazi, ili kuleta mabadiliko na ufanisi mahali pa kazi, ikiwemo mfumo wa kufuatilia utekelezaji wa mafunzo waliyopata kabla ya kupata uongozi.

Naye Mtendaji Mkuu TFS, Profesa Dos Santos Silayo amewapongeza wakufunzi waliotoa mafunzo hayo ya kijeshi na alishukuru bodi hiyo ya TFS na maelekezo ya Mwenyekiti huyo.

Amesema asilimia 98 ya watumishi hao wameshapitia mafunzo ya kijeshi na mafunzo hayo ni awamu ya kwanza kwa viongozi yanayohusisha kada mbalimbali za rasilimali za misitu, uhifadhi wa rasilimali nyuki, ikiwemo kukabiliana na changamoto za kiutendaji.

/* */