Makamu wa Rais Gambia afariki

Makamu wa Rais wa Gambia, Badara Alieu Joof amefariki akiwa nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu, Rais Adama Barrow amesema leo.

Hakuna taarifa za moja kwa moja za tatizo lililompeleka kutibiwa nchini India, kupitia ‘Tweet’ ya Rais Barrow imeeleza makamu wake amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.

“Hellow wana Zambia kwa moyo wa huzuni natangaza kuondokewa na makamu wa rais Badara Alieu Joof, tukio hilo la kuhuzunisha limetokea nchini India, badaa ya kuugua kwa muda mfupi.” imeeleza ‘tweet’ yake. haikusema alikuwa anaumwa ugonjwa gani.

Badara Alieu Joof aliyewahi kuwa waziri wa elimu aliondoka nchini Gambia kwenda India wiki tatu zilizopita kwa ajili ya kutibiwa ugonjwa uliokuwa ukimsumbua. Joof, 65, aliteuliwa kuwa makamu wa rais wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi mnamo 2022.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x