Makamu wa rais Ghana kugombea urais
CHAMA tawala cha New Patriotic Party (NPP) kutoka nchini Ghana kimemteua Makamu wa Rais, Mahamudu Bawumia kuwa mgombea wa uchaguzi wa urais wa utakaofanyika Disemba 2024, kikiandaa kinyang’anyiro na rais wa zamani John Mahama.
Mahamudu Bawumia, 60, ni mwanauchumi na aliwahi kuwa kamanda wa pili wa sera za kiuchumi katika kipindi chote cha urais wa Nana Addo Akufo-Addo anayetazamiwa kuachia ngazi Januari 2025 baada ya kutumikia nafasi yake kwa miaka minane.
Kiongozi huyo alipata asilimia 61 ya kura zilizopigwa katika hatua ya pili ya mchujo. Katika hotuba yake, Bawumia aliahidi kujenga upya uchumi uliokumbwa na mgogoro iwapo atachaguliwa kuwa rais.
“Nataka kuongoza taifa linaloboresha na kuibua vipaji vya vijana wetu na kutoa ajira nzuri zenye malipo mazuri na ukuaji endelevu wenye nidhamu ya uchumi mkuu.” alisema.