Makamu wa Rais wa uchumi Barcelona ajiuzulu

BARCELONA, Hispania: RAIS wa Barcelona Joan Laporta amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa Makamu wa Rais wa Uchumi wa klabu hiyo, Eduard Romeu kutokana na sababu zake binafsi.

Mapema leo Laporta alitoa taarifa ya klabu hiyo kuhusu kujiuzulu kwa Romeu huku akidai taarifa kamili za tukio hilo zitatolewa baadae lakini hakusita kumshukuru kwa utumishi wake mzuri katika kukuza uchumi wa klabu hiyo.

Katika taarifa inayotarajiwa kutolewa na rais huyo inatarajiwa kuwepo na mabadiliko ya kimuundo wa klabu hiyo huku mtu pekee akitajwa kuwa mrithi wa Romeu ni Angel Riudalbas ambaye anajina kubwa ndani ya Barcelona.

Timu ya Barcelona kwa sasa ipo katika hali mbaya ya uchumi inayowafanya watamani kuuza baadhi ya wachezaji wao ili kupata fedha za ambapo wanatarajia.

Barcelona wako tayari kumuuza Ronald Araujo msimu huu wa joto kwa euro milioni 100.

Mchezaji mwingine anayafikiliwa kuuzwa ni Jules Kounde ambaye ni mfaransa anayehitajika na timu nyingi za Ligi Kuu ya England katika majira ya joto.

Habari Zifananazo

Back to top button