Makanjanja kaeni chonjo msaada wa sheria wa Samia

NJOMBE: SERIKALI imewataka makanjanja kukaa chonjo, wakati ambao serikali imedhamiria kuwapelekea wananchi wataalamu bobezi, wenye weledi wa fani ya sheria ili kuwasaidia wananchi wasiojiweza kumudu gharama za mawakili katika kusimamia kesi zao.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) uliofanyika leo Mei 26, 2024 mkoani Njombe, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amewatoa shaka wananchi juu ya wataalamu watakaoletewa.

“Serikali itawaletea watu wenye uwezo siyo makanjanja,” amesema Biteko.

Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wananufaika na kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia wenye lengo la kuwapatia suluhu ya migogoro yao ya kila siku.

“Wote tukifanya kama jamii moja tutaunda taifa lenye umoja na furaha,” amesema.

Rejea: https://habarileo.co.tz/msaada-wa-kisheria-kwa-wanyonge-waja/

Naibu Mkuu huyo amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi pindi huduma hizi zitakapowafikia kwenye maeneo yao pia wasisite kushiriki kwa kuuliza maswali kwani wataalamu wapo tayari kuwahudumia.

Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7bYhO4uqMi/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

 

Habari Zifananazo

Back to top button