Makerere waadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa

Makerere waadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa

CHUO Kikuu cha Makerere kilichopo Uganda, kimeadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake kwa kutembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kutokana na kuwepo  uhusiano mzuri katika vyuo hivyo.

Naibu Makamu Mkuu wa UDSM anayeshughulikia utafiti, Prof. Bernadeta Kiliani, alisema hayo wakati wa maadhimisho hayo chuoni hapo.

Profesa Kiliani alisema maadhimisho hayo yamefanyika nchini Tanzania kwa kuwa vyuo hivyo vimekuwa na historia zinazofanana kwa kuanza kama  kama vyuo vishiriki London nchini Uingereza.

Advertisement

” Baadaye vyuo hivi vilikuwa vyuo vikuu vishiriki vya Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki,” alisema.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Makerere, Daniel Kidega, alisema wanajivunia wahitimu wawili chuoni kwao ambao wamekuwa marais wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Benjamini Mkapa.

Alisema marais hao wa Tanzania wamekuwa viongozi muhimu katika nchi yao na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Alisema dhumuni walilonalo ni kuandaa wahitimu watakaokuwa viongozi wakuu katika nchi hizo.

Naye Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa, Dk Ellen Mkondya- Senkoro, alisema chimbuko la uongozi bora wa marehemu Mkapa lilianzia Makerere Uganda.