Makomando watano wapotea Senegal

MAKOMANDO wanamaji watano wa Senegal wametoweka tangu Ijumaa wakati mashua inayoshukiwa kusafirisha dawa za kulevya ilipotegwa katika ufuo wa mji mkuu Dakar ilipokuwa ikitafutwa na jeshi la wanamaji, vikosi vya jeshi vinaeleza.

Boti ya doria ya Senegal ilikamata meli hiyo, inayoshukiwa kuhusika na biashara ambayo walanguzi wa dawa za kulevya husafirisha tani za kokeini kutoka Amerika Kusini hadi Ulaya, wakitumia nchi za Afrika Magharibi kama njia.

“Wakati wa msako huo, kikosi cha makomandoo wa baharini kilichokuwa kwenye meli kilibaini kuwa vali za meli zilikuwa zimefunguka,” vikosi vya jeshi vilisema.

“Kila kitu kinapendekeza kwamba hatua hii ya hujuma, inayojumuisha kuzama meli, ililenga kufuta ushahidi wote wa shehena hiyo haramu.”

Habari Zifananazo

Back to top button