Makombora Urusi yaleta hitilafu ya umeme Ukraine
RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amesema Ukraine inakusudia kubadili njia za umeme, ili kuleta utulivu katika gridi yake baada ya kuathiriwa na mashambulizi ya makombora ya Urusi jana.
Urusi jana ilirusha makombora yake katika baadhi ya maeneo hali iliyosababisha mikoa mingi kuathirika na upatikanaji wa umeme, huku mamlaka za mitaa zikionya kuwa karibu nusu ya Mkoa wa Kyiv utabaki bila umeme siku zijazo.
Makombora mengi yaligonga miundombinu ya umeme na makazi karibu na Mji wa Kusini wa Zaporizhzhia, maofisa wa mkoa walisema.
Watu wanne waliuawa katika mashambulizi ya Jumatatu. Ukraine sasa inakutana na chnagamoto ya joto kali katika maeneo mengi, na mamilioni hawana umeme na maji ya bomba. Kuna hofu kwamba watu kadhaa wanaweza kufa kutokana hali hiyo.
Katika hatua nyingine leo Jumanne, gavana wa eneo la Kursk nchini Urusi, amesema shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye uwanja wa ndege iliteketeza tanki la kuhifadhia mafuta.
“Hakuna majeruhi mpaka sasa,” alisema Roman Starovoyt. Hakusema wadhaniwa wa shambulio hilo katika eneo linalopakana na Ukraine.