Makombora yaua watu 20 soko Sudan

ZAIDI ya watu 20 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya makombora kurushwa katika soko la Omdurman kitongoji cha mji Mkuu wa Sudan Khartoum, kundi la wanasheria limeeleza.

Soko hilo linaloaminika kukusanya watu wengi lilipigwa baada ya majibizano makali ya risasi kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), Wanasheria wa Dharura wa Sudan, kundi lisilo la kiserikali, lilitoa taarifa hiyo.

Mawakili hao wamelaani pande hizo mbili zinazozozana kwa kuendeleza mapigano katika maeneo yenye wakazi wengi na kutaka kusitishwa kwa mapigano hayo.

Zaidi ya watu 9,000 wameuawa na wengine milioni tisa wamekimbia makazi yao tangu mapigano yalipoanza katikati ya mwezi April mwaka huu.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button