KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya CCM Taifa, Paul Makonda, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Binuru Shekidele kufungua stendi ya Mwembeyanga ambayo ilifungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Ametoa maagizo hayo wakati anazungumza na wananchi wa Kata ya Nyampulukano iliyopo Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
“Mkurugenzi naomba unisikie, leo naenda Mwanza nitalala pale, kesho saa sita stendi ifunguliwe haraka,” amesema Makonda.
Kuhusu changamoto ya kukosa hati ya ardhi kujenga soko, amemuagiza ofisa ardhi wa halmashauri ya wilaya hiyo kufuata hati hiyo Mwanza kesho kabla hajaondoka mkoani hapo.
Amesema msukumo wanaoweka kwa sasa n ikuhakikisha utekelezaji wa ilani unatakelezwa ipasavyo kwa uhakika.
Kiongozi huyo pia aliagiza kituo cha afya cha eneo hilo kifunguliwe haraka wiki ijayo, ili watu wapate huduma za afya, kwani sio vyema kutotoa huduma ikiwa tayari imekamilika kujengwa.
Pia amemuagiza Mkuu wa Wilaya kushirikiana na Walaka wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), wajenge barabara katika Kata ya Nyampulukano, ili kuondoa kero ya usafiri kwa wananchi.
Awali Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa katika jimbo hilo hivyo wanaendelea kumuunga mkono katika jitihada zake za kuijenga Tanzania.
Comments are closed.