Makonda awasha moto mafuriko Karatu

ARUSHA; Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameagiza uchepushwaji wa maji katika bwawa lililopo Mtaa wa Mangafi, Kata ya Karatu wilayani Karatu kuanza mara moja, ili kunusuru kaya zaidi ya 889 zenye watu 2800 zilizoathirika na mafuriko hayo.

Kutokana na bwawa hilo kujaa maji na kusabisha mafuriko, nyumba zaidi ya 31 zimebomoka, visima viwili vya maji kumezwa na kusbabishja watu 7,638 kukosa huduma hiyo, pamoja na transfoma kuharibika hivyo wananchi kukosa huduma ya umeme.

 

Agizo hilo la kuanza uchepushaji wa maji, limetolewa leo wilayani Karatu na Makonda baada ya kufika eneo la tukio na kujionea hali halisi ya nyumba kuzingirwa na maji, huku wananchi waliokumbwa na kadhia hiyo wakipewa hifadhi na majirani wengine.

Amesema haiwezekani wananchi watatu wakazuia uchepushaji huo, huku wenzao wengi wakikosa makazi na kwamba busara ni muhimu, hivyo uchepushaji wa maji hayo uanze mara moja na kuahidi msaada wa chakula na magodoro kusaidia wananchi hao.

Naye Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo, John Lucian amesema awali eneo hilo lilikuwa mashamba ambayo wananchi walikuwa wakilima na baadae mji ulipokua wananchi waliianza kujega eneo hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button