Makonda: Hatumdai Rais Samia

GEITA: KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini kwahiyo deni limebaki kwa wasaidizi wake kuhakikisha wanatekeleza miradi na kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa kero za wananchi wa Tanzania.
Makonda amesema hayo leo mkoani Geita wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Katoro waliojitokeza kumpokea na kueleza kero zao kwa kiongozi huyo
“Rais Samia Suluhu Hassan hana deni kwetu wananchi kwani ametoa fedha za kutosha za utekelezaji wa miradi mbalimbali kama ambavyo amekuwa akizitafuta, hivyo deni limebaki kwetu wasaidizi wake kuhakikisha tunafuatilia na kuweka msukumo kwa mamlaka husika zitekeleze wajibu wao juu ya miradi hiyo,” amesema
3 comments

Comments are closed.