Makonda na Waziri Mkuu wateta mazito

DODOMA: Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi, Paul Makonda amesema Chama hicho hakiwezi kutoa maelekezo yasiyotekelezeka na ndio maana  wameamua kutoa maelekezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwani kiongozi huyo ni mtekelezaji wa majukumu kwa wakati.

Novemba 02, 2023 Makonda amekutana na Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma ambapo ameeleza lengo la CCM ni kuhakikisha Serikali inatimiza kile ambacho imeelekezwa kukifanya kwa Ilani ya chama hicho.

“Tuna matumaini  makubwa na Waziri Mkuu, uzuri ni kwamba ni kada mwaminifu na mtiifu na maelekezo ya Chama ameyapokea na ameanza kuyafanyia kazi, na tunaamini  kwamba hata hiyo miezi sita ambayo Chama kimempa inawezekana akatumia miezi mitatu kutokana na kasi ya kiongozi huyo” amesema Makonda.

Advertisement

Makonda ameongeza kuwa kila atayekwamisha Ilani ya Chama hicho ni lazima achukuliwe hatua  na wamempa rungu Waziri Mkuu kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *