Makubaliano kusitisha vita yasogezwa mbele

GAZA, Palestina: MAKUBALIANO ya kusitisha vita ambayo yalisababisha kurejeshwa kwa wanawake na watoto 50 wa Kiisraeli kutoka Gaza, pamoja na makumi ya raia wengine, yameongezwa kwa siku mbili zaidi.
Maofisa walisema Jumatatu, huku mazungumzo awali ya siku nne yakikamilika kwa mafanikio kufuatia kutolewa kwa wafungwa usiku wa manane.

Waisrael 11 waliachiliwa huru na Hamas siku ya Jumatatu, Shirika la Msalaba Mwekundu na Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema, na kufanya jumla ya mateka walioachiliwa kuwa 69.
Wafungwa 33 wa Kipalestina pia waliachiliwa, na kufanya jumla ya wanawake na watoto wa Kipalestina kutoka magereza ya Israel kufikia 150.

Malori kadhaa ya mizigo ya misaada pia yalifika katika eneo hilo lililozingirwa katika kile ambacho kilikuwa ni mapumziko ya kwanza kwa Wapalestina katika takriban miezi miwili ya vita.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar Majed Al-Ansari alithibitisha kurefushwa kwa mapatano hayo katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wa X.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button