Makudubela, Maxi, Aziz Ki kuivaa Azam

YANGA SC imewasilisha majina ya wachezaji wa kigeni watakaokuwa sehemu ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC leo.

Hatua hiyo ni baada ya taarifa iliyotolewa leo Agosti 9, 2023 na shirikisho hilo ikidai kuwa ni Azam FC pekee ndio waliowasilisha majina ya wachezaji wa kigeni ambao watakuwa sehemu ya michezo ya Ngao ya Jamii.

Katika barua iliyotolewa na TFF imetaja wachezaji ambao Yanga imewasilisha majina yao kuwa ni, Maxi Mpia, Zouzoua Peodoh, Hafiz Konkon, Mahlatse Makudubela, Gift Fred, Koussi Yao, Kennedy Musonda, Khalid Aucho, Joyce Lomalisa, Stephane Aziz Ki, Jesus Moloko na Djigui Diarra.

Advertisement

Kwa mujibu wa TFF, Simba na Singida hawajawasilisha majina hadi sasa.

2 comments

Comments are closed.