Makumbusho ya taifa, UDART kuendeleza utalii malikale

MAKUMBUSHO ya Taifa la Tanzania imeingia makubaliano na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) kuendeleza utalii wa malikale Dar es Salaam, ikiwemo kutumia mabasi yake kutoa elimu kwa umma.

Makubaliano hayo pia ni katika kutangaza na kufanya ziara za kitalii kwenye urithi wa asili na utamaduni wa Tanzania unaohifadhiwa katika vituo vya makumbusho na malikale.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo Dar es Salaam katika kikao baina ya Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dk Noel Lwoga na Ofisa Mtendaji Mkuu wa UDART, Gilliard Ngewe pamoja na wataalamu kutoka Makumbusho ya Taifa la Tanzania na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka.

Kikao hicho kimefanyika katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Aidha, katika msimu wa sikukuu mashirikiano hayo yataanza kwa mabasi ya UDART kutangaza vivutio vya Makumbusho ya Taifa la Tanzania ili jamii ifahamu programu za utalii na kutembelea Makumbusho katika msimu huu wa likizo.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button