Makumbusho ya Taifa yanoga utalii wa ndani

Makumbusho ya Taifa yanoga utalii wa ndani

MAKUMBUSHO ya Taifa la Tanzania imeongoza kwa kuwa na watalii wengi wa ndani katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka 2023.

Taarifa ya takwimu za utalii kwa robo ya kwanza ya mwaka 2023, inayotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii inaonesha kuwa Makumbusho ya Taifa imepata watalii wengi wa ndani ukilinganisha na taasisi zingine za wizara.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano katika Taasisi ya Makumbusho, Joyce Mkinga, taarifa hiyo ya takwimu inayoonesha idadi ya watalii waliotembelea vivutio vinavyosimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, imeonesha Makumbusho ya Taifa ilitembelewa na wageni 219,627 katika kipindi husika.

Advertisement

Amesema taarifa hiyo imeongeza kuwa Makumbusho ya Taifa imeongoza katika utalii wa ndani kwa kupata watalii wengi wa ndani kupitia vituo vya Makumbusho ya Taifa ikiwemo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Kijiji cha Makumbusho, Azimio la Arusha, Makumbusho ya Elimu Viumbe, Makumbusho ya Majimaji, Makumbusho Mwl. J.K. Nyerere na Makumbusho ya Dk Rashid M. Kawawa pamoja na Mji Mkongwe wa Mikindani.

Taarifa hiyo inayotolewa na idara ya utafiti na mafunzo imeonesha kuwa ongezeko la watalii la asilimia 63.2, ukilinganisha na mwaka 2022, ambapo kipindi kama hicho taasisi ilipokea watalii wa ndani 134,603.

Amesema taasisi inayofuatia ni Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyopata watalii 177,146 katika kipindi husika, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ilipata watalii wa ndani 66,087, Wakala wa Huduma za Misitu iliyopokea watalii wa ndani 44,287 na TAWA iliyotembelewa na watalii wa ndani 11, 305.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *