Makusanyo ya madini Simiyu yafikia zaidi ya 103%

AFISA Madini Mkazi wa Mkoa wa Simiyu, Mayigi Makolobela, amesema mkoa huo umeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na Sekta ya Madini, ambapo makusanyo ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/2026 yamevuka malengo kwa kufikia zaidi ya asilimia 103 ya lengo lililowekwa kwa kipindi husika.
Akizungumza mkoani Simiyu, Makolobela amesema kwa mwaka wa fedha uliopita, ofisi yake ilipewa lengo la kukusanya Sh bilioni 4, lakini walifanikiwa kukusanya zaidi ya Sh bilioni 4.5.

“Kwa mwaka huu wa fedha tumewekewa lengo la kukusanya Sh bilioni 4.76, na hadi kufikia robo ya kwanza tayari tumekusanya zaidi ya Sh bilioni 1.23, sawa na asilimia 103 ya lengo la robo mwaka,” amesema Makolobela.
SOMA: Wazawa hawimizwa kuchangamkia fursa madini
Ameongeza kuwa tangu kuanza kwa Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, makusanyo ya madini kupitia wachimbaji wadogo mkoani humo yamefikia zaidi ya Sh bilioni 17, hatua inayodhihirisha ukuaji na uimara wa sekta hiyo katika Mkoa wa Simiyu.

Aidha, Makolobela amesema Simiyu ni miongoni mwa mikoa yenye utajiri mkubwa wa madini mbalimbali ikiwemo dhahabu, shaba, madini ya ujenzi, vito aina ya Amethyst na Nikeli yanayopatikana katika wilaya za Bariadi na Busega.
Hata hivyo, amebainisha kuwa tafiti za kina bado hazijafanyika ipasavyo katika maeneo yote ya mkoa huo, jambo linaloweza kusababisha baadhi ya maeneo yenye rasilimali kutobainika mapema.

“Kama Mkoa huu utafanyiwa utafiti wa kina, kuna uwezekano mkubwa wa kugundulika mashapo mengine, hususan madini ya metali yanayoweza kuchimbwa kwa kiwango cha kati na kikubwa, hivyo kuinufaisha Serikali na wananchi kwa ujumla,” amesema Makolobela.
Katika hatua nyingine, ameeleza kuwa Mkoa wa Simiyu una vituo vitano vya ununuzi wa madini pamoja na Soko Kuu la Madini lililopo Bariadi Mjini, ambapo shughuli kuu za biashara ya madini zinafanyika kwa ufanisi mkubwa.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Google pays $300 on a regular basis. My latest salary check was $8600 for working 10 hours a week on the internet. My younger sibling has been averaging $19k for the last few months, and he constantly works approximately 24 hours. I’m not sure how simple it was once I checked it out.
This is my main concern………. https://Www.Smartpay1.site