Malalamiko mengi ukiukwaji haki za binadamu, utawala bora

MALALAMIKO 1524  yaliyohusu uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora yaliwasilishwa Tume  ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB).

Waziri wa Sheria na Katiba, Damas Ndumbaro akiwasilisha bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma leo Aprili 25,2023 amesema hadi kufikia  Julai Mosi, 2022, THBUB ilikuwa na jumla ya malalamiko 1,524.

Amesema, kati ya hayo, malalamiko 725 yalihusu haki za binadamu na malalamiko 799 yalihusu utawala bora.

“Kati ya mwezi Julai 2022 hadi  Machi, 2023, THBUB ilipokea malalamiko mapya  123. Kati ya hayo, 39 yalihusu haki za binadamu na  84 yalihusu utawala bora.”Amesema

Aidha, amesema katika kipindi  hicho malalamiko yaliyofungwa yalikuwa 719, yote  ya miaka ya nyuma kati ya hayo,  malalamiko 318 yalikuwa ya haki za binadamu na  401 ya utawala bora. Hivyo kufanya idadi ya malalamiko yanayoendelea na uchunguzi katika hatua mbalimbali kuwa 928 kati ya hayo, malalamiko 446 yalikuwa ya  haki za binadamu na 482 ya utawala bora.

Habari Zifananazo

Back to top button