Malaria, homa ya mapafu bado tishio nchini

MALARIA, maambukizi katika mfumo wa hewa na maambukizi ya njia ya mkojo yametajwa kuongoza kuathiri zaidi wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu jana Mei 12,2023 mjini Dodoma ambapo amesema magonjwa hayo yamesababisha wananchi kwenda zaidi katika vituo vya kutolea huduma kupata matibabu.

Amesema, magonjwa yaliyoongoza hadi mgonjwa kulazwa hospitalini ni Malaria, homa ya mapafu na Anemia.

Aidha, takwimu zinaonesha kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza kwa kuwa ndani ya magonjwa kumi yanayoathiri zaidi wananchi.

 

Habari Zifananazo

Back to top button