KIWANGO cha maambukizi ya malaria kimepungua nchi ambapo mwaka 2008 takwimu zilionesha kuwa asilimia 18.1 walikuwa na malaria ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2022 ambapo kiwango kilikuwa 8.1.
Aidha vifo vitokanavyo na malaria vimeshuka kwa asilimia 76 kutoka vifo 6,311 vya mwaka 2015 hadi vifo 1,502 kwa mwaka 2022 huku waliothibitishwa kuwa na malaria wakipungua kutoka watu milioni 7.7 kwa mwaka 2015 hadi watu milioni 3.5 kwa mwaka 2022.
Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti na Kutokomeza Malaria Dk Abdalah Losasi alisema awali ni mikoa sita tu ilifanikisha kushusha kiwango cha malaria lakini sasa mikoa mitatu ya Songwa,Dar es Salaam na Mwanza yamefanikiwa pia na kufanya idadi kufikia tisa.
Dk Losasi alieleza kuwa maeneo ya Vijijini yanamaambukizi makubwa kwa asilimia 10.7 ilikinganishwa na maeneo ya mjini ambayo ni asilimia 0.7.
Alibainisha kuwa watu wenye hali duni ya maisha wanakubwa zaidi na malaria kwa asilimia 14.5 huku watu wanaoishi katika makazi bora kwa asilimia 0.6.
“Ingawa kuna mikoa ambayo inaonekana inamaambukizi ya juu kama Tabora ni asilimia 23.4 inaongoza ,Mtwara asilimia 20,Kagera 18 na Shinyanga 16 na Mikao iliyofanikiwa kushusha ni tisa ambazo ni Songwe,Dar es Salaam Mwanza,Arusha,Manyara,Kilimanjaro,Singida,Dodoma na Iringa .
Aliongeza “Tunahakikisha tunawafikia wote na kuchua takwimu lakini pia kuna changamoto za fedha zinakoseka tunaomba wadau wajitokeze kuchangia utekelezaji wa afua za malaria,lakini kwenye dawa ya unyunyiziaji wa viwadudu ni ghali sana halmashauri moja inatumia Sh bilioni 2 nani atachangi wadau wamechangi sasa wanajitoa,”alieleza.
Pamoja na hayo alisema wanafanya kazi ya kuelimisha kwa wanafunzi wa shule ya msingi wanawapa mafunzo na makundi mbalimbali na elimu ni endelevu wanaamini kadiri wanavyopata elimu wanabadilika .
Kuhusu Makazi duni amesema inaweza kuwa rahisi kupata magonjwa tofauti na Makazi bora ambayo yanapunguza magonjwa mengi sio malaria.
“Mtu anapokuwa na hali nzuri ya uchumi anapata kutazama familia ,anafatilia vyombo vya habari anaweza kupata habari kupitia mitandao taarifa zinamfikia haraka,”amesema.
Dk Losasi amebainisha kuwa hali ya Utoaji na umiliki wa vyandaru uko vizuri lakini matumizi ya vyandarua bado hayaridhishi na wanaendelea kupiga kampeni kuhamaishsa jamii watumie vyandarua kama ambavyo melekezo yanatolewa ili kuleta tija.
“Elimu ikitolewa itafanikisha kubadilisha tabia ya mwananchi sasa akibadili tabia atatumia na kumbadilisha mtu ni hatua wengine wanasema matumizi yake ni vyandarua,Mpango wa muda mrefu ni kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030.
Amesema mikakati ya wizara ya kwanza ni kuhakikisha wanapunguza wingi wa malaria na wanafua ambazo wanatarajia kufanya moja ni kutoa tiba kinga ya malaria kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja.
“Mama akienda kliniki anapewa dawakinga ya ASP pia mtoto anapewa kipande cha dawa ya ASP kwaajili ya kinga,Lakini pia tunataka kutoa tibakinga kwa watoto walioko shule ya msingi imebainika kuwa katika mikoa yenye maambukizi ya juu wanaishi na vimelea vya malaria ghafla mtoto unakuta jana yuko darasani na leo kalazwa hospitali na keshokutwa tumempoteza.
Ameeleza kuwa Dawa hizo tafiti zinaonesha zinaweza kusaidia kwa asilimia 80 kupunguza malaria na pia watatoa kwa watoto chini ya miaka mitano kwani wakilazwa wanakuwa na malaria wakipona baada ya muda akirudi anakuwa na upungufu wa damu.