Malipo madhara wanyamapori yaongezwa

DODOMA; Serikali imesema katika kipindi cha Julai 2023 hadi Mei, 2024, jumla ya Sh 2,400,258,500 zimelipwa kwa wananchi 10,552 waliopata madhara kutokana na wanyamapori wakali na waharibifu katika Halmashauri za Wilaya 48.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake mwaka wa Fedha 2024/2025.

Amesema wizara imefanya mapitio ya Kanuni za Kifuta Jasho na Kifuta Machozi za Mwaka 2011 kwa kuongeza viwango vya malipo kwa asilimia 50 kwa matukio ya majeraha ya muda, uharibifu wa mazao na vifo vya mifugo na asilimia 100 kwa majeraha ya kudumu na vifo.

Habari Zifananazo

Back to top button