Malipo ya Kombe la Dunia yasaidie wenye uhitaji – Rudiger

BEKI wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ujerumani, Antonio Rudiger ameanza kampeni za mashindano ya kombe la dunia kwa staili ya kipekee, baada ya kuagiza fedha zote atakazolipwa Kombe la Dunia ziende kwa watato wenye mahitaji.
Kundi la watoto 11 wenye mahitaji, wanaoishi nchini Sierre Leone watanufaika na msaada huo.
Kwa ushirikiano na shirika la misaada la Ujerumani BigShoe, kama alivyofanya Januari mwaka jana, beki huyo wa Real Madrid amefadhili mfululizo wa matibabu gharama kubwa na muhimu zaidi ya kubadilisha maisha ya watoto.
–