RAIS wa Marekani, Joe Biden, ameandika katika ukurasa wake wa Twitter, akisema Malkia Elizabeth II wa Uingereza, ataendelea kukumbukwa kwa upole na ukarimu wake.
“Tulikutana na Malkia kwa mara ya kwanza mwaka wa 1982, na daima tutakumbuka wema na ukarimu wake..,” Rais wa Marekani, Joe Biden, ambaye ameambatana na mke wake, Jill Biden, aliandika kwenye ukurasa wake.
Malkia Elizabeth II alifariki Septemba 8, 2022 na Mazishi yake yatafanyika leo Septemba 19, 2022 jijini London.
Ibada ya mazishi yake itafanyika Westminster Abbey na kisha mwili wa marehemu kupelekwa kasri la Windsor kwa ibada ya kifamilia na watu wa karibu zaidi, hatimaye, maziko ya kibinafsi.
Jumla ya wageni 2000, viongozi 500 wa kigeni, wahudumu 4,000 watashiriki na mabilioni ya watu duniani kote wanatarajia kufuatilia maziko yake leo.