Malkia wa Uingereza, Elizabeth wa II amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96.
Amekalia kiti hicho kwa miaka 70 na anatajwa kuwa ndiye mtu aliyetawala Uingereza kwa muda mrefu zaidi ikilinganishwa na watangulizi wake.
Kabla ya kutangazwa kwa taarifa hizo, familia yake ilikusanyika baada ya uvumi kusambaa juu ya utata wa afya yake.
Aliingia madarakani mnamo mwaka 1952 na katika kipindi hicho , BBC inasema, Elizabeth II ameshuhudia mabadiliko mengi ya kijamii.
Kutokana na kifo hicho, mtoto wake mkubwa wa kiume, Charles, mwanamfalme wa zamani wa Wales ataliongoza taifa hilo katika kuomboleza kifo cha mama yake kama Mfalme mpya. .
Taarifa ya Kasiri la Buckingham imenukuliwa ikisema: “Malkia amefariki kwa amani jioni hii huko Balmoral.”